Kartra

Kocha Ajiondoa Man Utd Kisa Vifaa Vibovu


KUKOSEKANA kwa vifaa muhimu kwa ajili ya mazoezi kumetajwa kuwa chanzo cha Casey Stoney kuamua kujiondoa katika majukumu ya kuinoa timu ya soka ya wanawake ya Manchester United.

Stoney, ambaye amekuwa akiinoa timu hiyo tangu mwaka 2018, amekuwa hana furaha na vifaa na miundombinu wanavyotumia wachezaji wake kwenye viwanja vya mazoezi vya Carrington, huku wapinzani wao, Man City wakidaiwa kuwa na mazingira mazuri.

United hawajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo lakini tayari kocha huyo amewasilisha barua yake na ataondoka baada ya msimu huu kumalizika.


Toa comment