The House of Favourite Newspapers

Kocha Ndanda Apanga Kuwavuruga Yanga SC

0
Kikosi cha timu ya Yanga.

KOCHA Msaidizi wa Ndanda FC, Musa Mbaya ‘Moloto’ amefunguka kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wao dhidi ya Yanga bila ya kuhofia majina wala ukubwa wa timu hiyo.

Yanga na Ndanda zinatarajiwa kupambana Jumamosi wiki hii kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Moroto alisema kutokana na ubora wa timu yake hawawezi kuwahofia wapinzani wao kwa kuwa malengo yao ni kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo ili kujiweka kwenye mazingira bora zaidi.

 

“Tupo vizuri, tumeweka kambi ya muda mfupi Morogoro kwa ajili ya mechi hiyo na kikubwa tunataka kuhakikisha tunaibuka na ushindi dhidi ya wapinzani wetu, Yanga ni timu kubwa zaidi yetu lakini hatuwezi kuwahofia kwa sababu Ndanda nayo ni kubwa na ndiyo maana inacheza ligi kuu.

 

“Mechi za Dar dhidi yao kwetu zinakuwa hazina matokeo mazuri lakini Ndanda haichagui wapi kwa kucheza naamini tutapata matokeo ya kushangaza timu ipo vizuri, huko tumepanga kuja kesho (Alhamisi kwa kuwa bado tunamalizia mambo yetu,” alisema Moroto.

Leave A Reply