testiingg
The House of Favourite Newspapers

Kocha wa Simba Akomaa Na Ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga Inaongoza Ligi

0
Kocha Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda (kushoto) na kulia wachezaji wa timu ya Simba.

KOCHA Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda, amesema kuwa timu yao bado ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu kwani michezo iliyobaki ni mingi.

Mgunda alisema, ligi ni kama mbio za vijiti, mnakimbia kwa kupokezana, hivyo wao wataamini kuwa ubingwa wameukosa pale ambapo ligi hiyo itafikiwa ukomo.

Kauli ya Mgunda imekuja wakati hivi sasa Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 65, imeiacha Simba pointi nane ikiwa nafasi ya pili ikikusanya pointi 57. Timu zote hizo zimebakiwa na mechi sita, huku moja kati ya hizo, wakicheza wenyewe.

Akizungumza na Spoti Xtra kwa kujiamini sana, huku akiachia tabasamu, Mgunda alisema: “Haijaisha mpaka iwe imesha kabisa, malengo yetu kwenye ubingwa bado yapo palepale na tunaiona hiyo nafasi.

“Nasema hivyo kwa sababu bado kuna mechi nyingi zimebaki, timu ambayo inaongoza ligi imetuacha alama ambazo ukitazama lolote linaweza kutokea, bado tupo kwenye mbio za ubingwa na tunautaka.”

MAPITO ya IMELDA wa GLOBAL TV, KUTIMULIWA na WALINZI wa DIAMOND, UGOMVI na WEMA, MIAKA 21 OFISINI..

Leave A Reply