The House of Favourite Newspapers

Koffi afunguka unyanyasaji wanawake kingono

0

PAMOJA na Mahakama ya Rufaa nchini Ufaransa kumuondolea mwanamuziki Koffi Olomide wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kosa la unyanayasaji wa kingono, lakini imemtia hatiani kwa kuwashikilia wanawake bila hiari yao.

Mahakama ilibatilisha uamuzi wa mwaka 2019 uliomtia Koffi hatiani kwa ubakaji wa mmoja wa wanenguaji wake alipokuwa na umri wa miaka 15.

Lakini alipatikana na hatia ya kuwanyima wanawake uhuru wao katika jumba la kifahari huko Paris, Ufaransa kati ya mwaka 2002 na 2006.

Hivyo atatumikia kifungo cha miezi 18 kilichoahirishwa kwa muda na kuwalipa fidia.

Hata hivyo, wakati hayo yakiendelea, shirika moja la habari limetoa makala ya mahojiano lililofanya na Koffi ambaye alikanusa kuhusika na unyanyasaji wa kingono wa wanawake.

Mtaalam huyo wa Rhumba alikanusaha tuhuma zote zinazoelekezwa kwake juu ya unyanyasaji wa wanawake hivyo kuandamwa na msururu wa kesi za sampuli hiyo.

“Si kweli, yote si kweli!” Alisema Koffi.

Nguli huyo wa muziki barani Afrika mwenye umri wa miaka 65, mwaka 2019 alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la unyanyasaji wa kingono kwa mabinti wadogo.

Akizungumzia hukumu hiyo, Koffi alisema; “Inashangaza kwa namna f’lani…”

Katika kesi hiyo, wanawake wanne wa Kongo waliwasilisha ushahidi wao wa vitendo hivyo walivyofanyiwa na mwamba huyo kati ya mwaka 2007 na 2013, wakiwa ni wanenguaji wake.

“Ni sinema,” alisisitiza Koffi kwenye mahojiano hayo.

STORI; ELVAN STAMBULI, DAR

Leave A Reply