The House of Favourite Newspapers

Koffi Apigwa Stop Rwanda

0

Wanaharakati wa haki za wanawake nchini Rwanda wamelipiga ‘stop’ tamasha la mwamba wa Rhumba wa Congo, Koffi Olomide kwa tuhuma za ubakaji na unyanyasaji wa kingono anazokabiliwa nazo katika Mahakama za Ufaransa.

 

Mwezi Desemba, Mahakama ya Paris nchini Ufaransa itatoa uamuzi wa rufaa iliyoombwa kwa mashtaka dhidi ya Le Grand Mopao Mokonzi ambaye alipatikana na hatia ya kuwanyanyasa kijinsi wanenguaji wake wanne wa zamani.

 

Juliette Karitanyi, mwanaharakati mjini Kigali, Rwanda anasema kumruhusu Koffi kutumbuiza nchini Rwanda itakuwa ni kutoheshimu waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono.

 

Hata hivyo, baadhi ya watetezi wa Mopao Mokonzi kwenye mitandao ya kijamii wanasema hakuna msingi wa kisheria wa kumzuia kutumbuiza nchini Rwanda.

STORI NA SIFAEL PAUL | GPL

RAIS SAMIA ANAMPOKEA RAIS MUSEVENI WA UGANDA AIRPORT DSM MUDA HUU..

Leave A Reply