The House of Favourite Newspapers

Koffi Olomide Ahukumiwa Kwenda Jela

0

MAKAHAMA ya rufaa ya Versailles nchini Ufaransa imemfutia shitaka la unyanayasaji wa kingono na kumtia hatiani kwa makosa ya kuwashikilia wanawake bila riddhaa yao mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi, Koffi Olomidé kutokea nchini Congo DR.

 

Mahakama hiyo ilibatilisha uamuzi uliotolewa mwaka 2019 uliomkuta na hatia ya ubakaji wa mmoja wa wanenguaji wake alipokuwa na umri wa miaka 15 pamoja na madansa wengine wanne.

 

Lakini Mopao au Papa Ngwasuma alipatikana na hatia ya kuwanyima wanawake uhuru wao katika jumba la kifahari, Asnières huko Paris, kosa ambalo alilitenda kati ya mwaka 2002 na 2006.

 

Baada ya kumkuta na hatia hiyo, mahajama imemuhumu Koffi kifungo cha miezi 18 na kuwalipa fidia ya dola $11,000-36,000 (sawa na Tsh milioni 25.344 mpaka Tsh milioni 82.944) kwa kila mcheza dansa.

 

Wakati akijitetea, Mopao alisema binti huyo alikuwa na nia ya kuishi nchini Ufaransa ili afanye kazi katika mashirika na kulipwa ujira lakini yeye kama msanii amekuwa akiwalea vizuri mabinti na wanawake anaofanya nao kazi bila kuwabughudhi.

 

Hivi karibuni, Mopao alipigwa marufuku kufanya matamasha yake katika nchi za Rwanda na Kenya. Miaka michache iliyopota, alipigwa marufuku kufanya tamasha lake nchini Kenya baada ya kuonekana akimpiga mateke mnenguaji wake wa kike wakati waliposhuka katika Uwanja wa ndege.

Leave A Reply