The House of Favourite Newspapers

Koletha Alizwa

0

colethaStori: Gladness Mallya

MSANII mkongwe kwenye gemu la filamu Bongo, Koletha Raymond amejikuta katika wakati mgumu baada ya kulizwa zaidi ya shilingi laki tano na mfanyakazi wake.

Akipiga stori na paparazi wetu, Koletha alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Lion-Sinza, Dar  kwenye pub yake ambapo mfanyakazi wake anayejulikana kwa jina la Anna aliyekuwa mhudumu aliyekusanya fedha za mauzo za siku tatu ambazo Koletha hakufika kazini na kuondoka nazo.

“Yaani nilihisi kuchanganyikiwa kwani siku tatu sikufika hapo pub, siku niliyofika nikakuta friji la vinywaji liko tupu na kwenye droo hakuna hela yoyote, nimekuwa nikimtafuta sana huyo msichana lakini hapatikani kwenye simu na anapokaa amehama, nimeamua kumwachia Mungu tu maana naona nikienda polisi nitakuwa napoteza muda wangu bure, nimeamua kuuza mwenyewe hapa pub kwangu maana hii siyo mara ya kwanza kuibiwa,” alisema Koletha.

Leave A Reply