The House of Favourite Newspapers

Kongamano la Victory Campus Night 2019 Latikisa Dar! – Video

HATIMAYE lile kongamano la kimataifa linalowakutanisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, Victory Campus Night la mwaka 2019, limefanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na umati  uliofika kwa ajili ya kumshukuru Mungu na kukutana na marafiki.

 

Tamasha hilo lililoandaliwa na Kanisa la VCCT – Mbezi Beach, chini ya mchungaji Dkt. Huruma Nkone, limetikisa Jiji la Dar es Salaam ambapo  licha ya mvua kunyesha,  watu walijaa uwanjani na ratiba ikaenda kama ilivyokuwa imepangwa.

Katika tamasha hilo, ambalo lilianza majira ya saa 1:00 jioni, waimbaji mbalimbali walipanda jukwaani kuimba wakimsifu Mungu, baadhi yao wakiwa Upendo Nkone, Miriam Lukindo Mauki, Joel Lwaga, Kwaya ya Uinjilisti ya Kijitonyama, Ipyana Kibona, Mkhululi Bhebhe kutoka nchini Afrika Kusini na wengine wengi.

Mbali na burudani hizo pia kulikuwa na Neno la Mungu kutoka kwa Mchungaji, Dkt. Huruma Nkone,  ambaye amewaasa vijana na kuwapa moyo wa kuendelea kupambana huku wakimfuata Mungu na kuachana na matendo yanayomchukiza muumba wao.

Aidha, katikaai ya shughuli hiyo,  kuliibuka ‘sapraizi’ ya ugeni wa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, ambao pia walipata wasaa wa kuwashauri wanafunzi hao waliokuwa wamehudhuria kongamano hilo. Makonda amewataka kutokata tamaa kwani hakuna anayejua mwisho wa maisha yake.

Amewaeleza kuwa hata yeye alitoka kwenye maisha duni ya umaskini,  hali iliyosababisha kufukuzwa kwenye nyumba aliyokuwa amepanga maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar, lakini Mungu amemuinua mpaka leo amekuwa Makonda ambaye wengi wanamfahamu.

PICHA NA RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERS

TAZAMA TUKIO ZIMA HAPA

Comments are closed.