Kopa, Msagasumu Kupamba Shindano la Nyonga

WAMAMA wa uswazi na ushuwani leo Alhamisi wanata-rajiwa kuon-eshana matu-mizi ya nyonga kwenye shindano litakalo-fanyika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na gazeti hili, mratibu wa tamasha hilo, Maimartha Jesse alisema shindano hilo litasind-ikizwa na burudani kutoka kwa Mfalme wa Uswazi (Msaga-sumu), Malkia wa Mipasho (Khadija Kopa), Jack Simela na wengineo.

 

Sambamba na wasanii hao Maimartha alisema pia kutakuwa na burudani ya ngoma za Kibao Kata na Baikoko kutoka Tanga.

Maimartha alisema upande wa ushereheshaji atakuwa yeye mwenyewe akisaidiana na Sakina Liyoka ambao kama kawaida yao watamwaga ubuyu mwanzo mwisho. Katika burudani zote hizo kiingilio kitakuwa shilingi 5000 tu.

RICHARD BUKOS
Toa comment