The House of Favourite Newspapers

Kubenea Akamatwa kwa Tuhuma za Utakatishaji Fedha

0

ALIYEKUWA Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea, amekamatwa na Jeshi la Polisi katika mpaka wa Tanzania na Kenya, Namanga, akidaiwa kuvuka mpaka usio rasmi na kuingiza nchini fedha za kigeni bila kuwa na kibali maalum.

 

Katika taarifa iliyotolewa leo Septemba 7, 2020 na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Kubenea alikamatwa Septemba 5, 2020 akitokea nchini Kenya na baada ya upekuzi, alikutwa na Dola za Kimarekani 8,000, fedha za Kenya kiasi cha shilingi 491,000 na fedha za Kitanzania shilingi 71,000.

 

Taarifa hiyo inaeleza kwamba Kubenea atapandishwa kizimbani akikabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha na kuvuka mpaka usio rasmi.

 

Leave A Reply