The House of Favourite Newspapers

Kuelekea Derby Ya Kariakoo Ali Kamwe Aipania Simba Kuikanda 5G Tena – Video

0
Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe

Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema Kuelekea mchezo wao wa Derby ya Kariakoo Jumamosi, sisi Yanga hatuiangalii Simba kama nyie wengine mnavyoiangalia, sisi tunaingalia Simba kama timu Tishio na tunayowania nayo Ubingwa.

Ni timu yenye wachezaji wazoefu na Viongozi wazuri na ndio maana sisi kama Young Africans SC haendi kwenye Derby kwa kuwaangalia Simba kama ambavyo waandishi na watu wengine wanavyoiangalia”

“Sisi kama Young Africans tumeamua mchezo huu wa Jumamosi tuwakabidhi Wazee wetu, huu mchezo wa Derby wa Jumamosi ni , Wazee wa Yanga wote hii mechi ni ya kwenu, tukifungwa ni nyie.

Tunaomba mkatuheshimishe wazee wetu, mje kwa wingi Benjamin Mkapa lakini tunaamini pia kupitia Dua zenu tutafanya vizuri”

“Viingilio vya mchezo Kariakoo Derby Jumamosi ni kama vifuatavyo;

VIP A – 50,000
VIP B – 30,000
VIP C – 20,000
MACHUNGWA – 10,000
MZUNGUKO – 5,000

Leave A Reply