The House of Favourite Newspapers

Kumbe Ini Edo hakuwa mjamzito!

0

ini edo.jBAADA ya habari kusambaakwa muda wa miezi miwili kwenye mitandao mbalimbali kuwa mkongwe wa fi lamu Nollywood, Ini Edo ni mjamzito imebainika kuwa taarifa hizo hazikuwa na ukweli.

Kwa mujibu wa mtandao mmoja nchini Nigeria ambao ulifanya mahojiano na rafi ki wa karibu wa Ini, mkongwe huyo hakuwa na ujauzito kama ilivyozushwa.

“Hata ukiangalia katika mitandao yake ya kijamii kila siku anaendelea kuweka picha zake zikimuonesha umbo lake lote ambalo halioneshi dalili zozote za ujauzito na bado yupo Nigeria,” alisema mtu huyo.

Hivi karibuni mitandao mingi iliandika juu ya Ini Edo kuwa na ujauzito ambao haikufahamika baba ni nani. Ilidaiwa kuwa astaa huyo alikuwa na mpango wa kuhama nchini kwao na kwenda kujifungulia kati ya Uingereza ama Marekani.

Leave A Reply