The House of Favourite Newspapers

Kumbe! Mimba ya Shamsa Imechoropoka

KUMEKUWA na matukio mbalimbali yanayowakusanya wasanii, lakini tofauti na zamani, Shamsa Ford kwa sasa amekuwa haonekani akijichanganya na wenzake, jambo ambalo limezua minong’ono na kusababisha mwenyewe kuibuka na kudai kuwa jambo hilo lilisababisha mimba yake changa ikachoropoka.

 

Shamsa aliiambia Za Motomoto News kuwa, awali alikuwa akijichanganya mno kwenye ishu tofauti, lakini kwa sasa anashindwa kutokana na kupigwa marufuku na mumewe, Chid Mapenzi, baada ya kuwa na ujauzito mchanga ambao ulichoropoka kwa sababu ya kuzurura.

 

“Nilipigwa marufuku kutokatoka licha ya kwamba mwanzoni nilikuwa ninatoka kibishibishi tu, lakini kwa sasa imenibidi nimsikilize mume wangu zaidi maana mimba changa ilitoka kwa sababu ya kutokatoka hovyo kwenda kwenye shughuli,” alisema Shamsa.

ZIMEANDALIWA NA GLADNESS MALLYA

Comments are closed.