Kumbe mjengo wa P Diddy mgumu kuuzika!
P Diddy
IMEBAINIKA kuwa mjengo wa rapa wa Marekani, Sean Combs a.k.a P Diddy uliopo jijini New York ambao uliwekwa sokoni wiki iliyopita kwa shilingi bilioni 13 mgumu kuuzika.
Mjengo wa P Diddy
P Diddy ambaye ni rapa tajiri zaidi duniani kwa mujibu wa orodha ya Forbes akiwa na utajiri wa zaidi ya trilioni moja, mwaka 2012 alitaka kuuza mjengo huo uliopo ghorofa ya 66 kwenye jengo la Park Imperial kwa shilingi bilioni 17 ukashindikana, mwaka 2013 akauweka tena sokoni kwa shilingi bilioni 15 napo ukashindikana na mwaka huu ameshusha tena kwa bilioni 13 napo inaonekana ngumu kuuzika.
Inaelezwa kuwa alinunua mjengo huo mwaka 2005 kwa shilingi bilioni 6.