The House of Favourite Newspapers

Kumbilamoto Meya Mpya Jiji la Dar – Video

0

RAIS John Magufuli amesema Halmashauri ya Manispaa ya Ilala inastahili kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, na haijapendelewa kwani hata katika mapato wanaongoza huku akielekeza kuwa Mstahiki Meya wa Ilala ambayo jana ilipandishwa hadhi na kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar pamoja na Naibu Meya wanastahili kuwa Mameya wa Jiji hilo.

 

 

Akizungumza katika Mkutano wa Hadhara wa Rais Magufuli uliofanyika Mnazi Mmoja Dar es Salaam,  ametoa wito kwa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuwa waaminifu katika kazi zao.

 

 

 

“Nawapongeza sana Watu wa Ilala kwa Manispaa ya Ilala kuwa Jiji la Dar es salaam, hongereni sana, mnastahili wala hamkupendelewa, hata kwenye taarifa iliyotolewa na Waziri inaonekana mnaongoza kwa mapato, sasa kwa nini mlinganishwe na Manispaa Manispaa!?

 

 

“Kwa nini Meya wa Manispaa ya Ilala inayoongozq kwa mapato Nchi nzima alinganishwe na Meya wa Manispaa nyingine? Meya wa Ilala na Naibu wako mnastahili kuwa Mameya wa Jiji la DSM, najua Watu walikuwa wanatazama nafasi hiyo, hakuna kugombea, wewe ndiye Meya wa Jiji la Dar.

 

 

“Meya wa Ilala na Naibu wako nyinyi ndio Maboss wa Jiji la Dar, na nyinyi Madiwani ndio Madiwani wa Jiji, baadhi ya Barabara ni mbovu kwasababu mlikuwa mnalinganishwa mapato na Manispaa nyingine sasa bajeti yenu itakuwa kubwa hamuwezi kulinganishwa na Kino, Kigamboni au Temeke.

 

 

“Najua watu walikuwa wanatazama nafasi hiyo, wengine wakiwa wamejipanga kugombea. Hakuna cha kugombea wewe ndio Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,” amesema.

 

 

 

Amesema kuna watumishi huwa wanawakadiria wafanyabishara kodi kubwa sana na wanaposhindwa kulipa basi hutaka kugawana kile kiasi kidogo ambacho mfanyabiashara anakuwa nacho.

 

 

Amewataka TRA wajifunze kutoa haki kwa wafanyabishara ambao wanania ya kulipa kodi. Amesema TRA kuna wafanyakazi wala rushwa, hivyo ni lazima wajirekebishe na kuiambia Wizara ya Fedha kuwa wakasimamie suala hilo, kwa kuwa nchi inahitaji kodi, inahitaji ushuru lakini uwe wa haki.

 

 

Leave A Reply