The House of Favourite Newspapers

Kupatwa kwa jua, Profesa Bisanda ataja faida zake

0

1. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania, Prof. Elifasi Bisanda (kulia) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania, Prof. Elifasi Bisanda (kulia) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

2. Mhadhiri wa Fizikia Katika Kitivo cha Sayansi na Elimu ya Mazingira katika Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania ambaye pia ni Mtaalamu wa Astronomia, Dkt. Noorali Jiwaji akionesha chujio la mwanga.

Mhadhiri wa Fizikia Katika Kitivo cha Sayansi na Elimu ya Mazingira katika Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania ambaye pia ni Mtaalamu wa Astronomia, Dkt. Noorali Jiwaji akionesha chujio maalum za mwanga.

3

Mkutano ukiendelea.

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof. Elifasi Bisanda, amesema kuwa Watanzania wanapaswa kuelekeza macho yao katika tukio kubwa la anga na la kipekee la kupatwa kwa jua usawa wa Tanzania litakalotokea Septemba Mosi, mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Bisanda amesema tukio hilo litaanza majira ya saa 4:17 asubuhi hadi 7:56 mchana, hivyo wataalamu wa anga kutoka duniani kote, wanasayansi, wanafunzi na wananchi wengine wataweza kuona vizuri tukio hilo wakiwa maeneo ya Rujewa mkoani Mbeya.

Bisanda ameeleza kupatwa kwa jua ni kitendo cha kivuli cha mwezi kuangukia dunia na kuwa kidogo.

Kwa upande mwingine, Bisanda amesema wanategemea kusambaza chujio maalum za mwanga ili watu wengi waweze kuona tukio hilo.

Aidha Bisanda alisema kutokana na tukio hilo, wanafunzi wataweza kupata somo kwa vitendo jinsi Sayansi ya Astronomia na kuelewa namna jua, mwezi na dunia zilivyopangika angani hadi kusababisha kupatwa.

Vilevile Bisanda alifafanua kuwa nchi inaweza kufaidika kiuchumi kutokana na tukio hilo endapo watalii kutoka nchi za nje watakuja kushuhudia tukio hilo huku akitolea mfano wa Bara la Amerika ambalo lilishaanza kutangaza tangu mwaka jana tukio lao la kupatwa kamilifu kwa jua la Agosti, mwakani ili wapate watalii wengi pamoja na kuhamasisha watu wao kuifaidi msisimko wa tukio hilo.

Pia Bisanda alizitaka taasisi zote za elimu kujitayarisha kwa ajili ya siku hiyo ili walimu watakaopenda waweze kuwaongoza vyema wanafunzi wao katika Somo la Astronomia.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply