The House of Favourite Newspapers

KUTOKA MAN U KWENDA EVERTON, ROONEY ON FIRE!!

0
ROONEY ON FIRE
Rooney.

WAYNE Rooney, mshambuliaji wa Klabu ya Everton ya England ni kama anamuumbua kocha mwenye maneno mengi wa Manchester United, Jose Mourinho. Mourinho, ambaye mkataba wake wa kuinoa Chelsea kwa mara ya pili ulikatishwa mwaka 2015 kutokana na matokeo mabovu, alichukuliwa na Manchester United mwaka uliofuata na kitu cha kwanza alichokifanya kocha huyo Mreno, ni kumleta kikosini, mshambuliaji Msweden, Zlatan Ibrahimovic, aliyekuwa amemaliza mkataba wake PSG.

 

Mourinho aliingia United akimkuta Rooney akiwa tegemeo la kikosi hicho katika kupachika mabao kwa miaka kumi mfululizo, tangu alipojiunga na mashetani hao wekundu akitokea klabu iliyomkuza ya Everton kwa ushawishi wa kocha wake wa wakati huo, Sir Alex Ferguson.

 

Tangu anawasili, Mourinho hakuonekana kuwa na mipango na Muingereza huyo mzaliwa wa jijini Liverpool na kuthibitisha hilo, akaanza kumtumia kwa nadra mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 35, ambaye aliifanya kazi yake vizuri kiasi cha kufunga mabao 28 katika michuano yote katika msimu wake wa kwanza na United KUCHEZA kwa Zlatan, kulimaanisha kukaa benchi kwa Rooney, kitu ambacho kilionyesha wazi kuwa siku za nahodha huyo wa timu ya taifa ya England kikosini, zilikuwa zikihesabika.

 

Sura ya mshambuliaji huyo akiwa benchi, ilikuwa na ujumbe mmoja tu, kutoipenda hali hiyo. Na kitu hicho kikaleta hisia nyingi juu ya mchezaji huyo ambaye wakati fulani aliishi kama mfalme katika vyumba vya kubadilishia nguo ndani ya Old Trafford, kitu kilichochangiwa na historia yake ya kutwaa vikombe vyote ambavyo klabu hiyo ilishiriki. Alishachukua Ligi Kuu England, FA, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Ligi, Kombe la Europa na Kombe la Dunia la Klabu.

 

Hapo ndipo zikaanza kuzaliwa hisia za Rooney kuihama klabu hiyo aliyoichezea kwa mafanikio makubwa, wengine wakimhusisha na klabu za China, ambako waliamini katika umri wake wa miaka 31, alistahili kwenda kuvuna mapesa katika ligi hiyo inayokuzwa huku wengine wakimhusisha pia na ligi ya Marekani, ambako pia ni sehemu ya kwenda kupata fedha tu, kwani viwango vya soka vipo chini kulinganisha na Ulaya, hasa England.

 

Rooney alikaa kimya pasipo kuzungumza mwelekeo wake hadi karibia na mwishoni mwa usajili wa majira ya joto alipotangaza kurejea klabu yake ya toka utotoni ya Everton. Ni kama walibadilishana na mshambuliaji nambari moja wa klabu hiyo ya Meseyside, Romelo Lukaku ambaye alijiunga na Man United.

 

Kwa mara ya kwanza Rooney alijiunga na Everton akiwa na umri wa miaka 9 na
Stamford Bridge kwa mara ya pili. Mata alijiunga na United na haikudhaniwa kama angeweza kumtumia akiwa Old Trafford, lakini makali ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania, yamemfanya awe mmoja wa wachezaji anaowategemea katika timu yake kwa sasa.

 

Lakini moto mpya wa Rooney, akiwa katika klabu yake mpya ya Everton, siyo kitu cha kufurahisha kwa Mourinho, kwani linaweza kuwa jambo ambalo linaweza kumletea matatizo na mashabiki, hasa kama United itakuwa na msimu mwingine mbaya chini yake.

 

Akiwa katika kiwango chake bora kabisa, Rooney aliisaidia Everton kupata ushindi wake wa kwanza katika mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu England, alipofunga bao la ushindi kwenye mchezo dhidi ya Stoke City na alifunga bao jingine la kuongoza wakati vijana hao wa Goodison Park walipotoka sare ya 1-1 na Manchester City, iliyolazimika kupigana kufa na kupona ili kuokoa pointi moja.

 

Kwa kufunga kwake mara mbili mfululizo, ni wazi kuwa inamjengea kujiamini sana na huenda akafanya vizuri kuliko ilivyotegemewa. Kuwekwa kwake benchi akiwa United, kulikuwa kunampa wakati mgumu kutetea nafasi yake katika kikosi cha timu ya taifa, lakini kwa jinsi alivyocheza katika michezo hiyo miwili, ni wazi kuwa heshima yake kama nahodha inarejea.

 

Kwa vyovyote, Rooney atakuwa akiingia uwanjani kujaribu kuonyesha mashabiki kuwa Mourinho alikuwa akikosea kumweka nje na kama nilivyosema pale juu, endapo United itakutana na msimu mwingine mbaya, kocha huyo wa zamani wa Juventus anaweza kujikuta matatani kutoka kwa mashabiki. Hata hivyo, msimu huu unaweza kuwa mzuri kwa United, kwani katika mechi zake mbili za kwanza, imefanya vizuri asilimia 100, kwani imeshinda kwa 4-0 katika michezo yake yote na inashikilia usukani katika Ligi Kuu England, angalau hadi kesho jioni!

 

Akaichezea mechi yake ya kwanza katika timu ya wakubwa akiwa na umri wa miaka 16, hiyo ikiwa ni mwaka 2002, lakini mwaka 2004, akaondoka na kujiunga na United, akiwa amecheza mechi 67 na kukwamisha mabao 15.

 

Alipojiunga na United, katika miaka yake zaidi ya kumi, Rooney aliichezea klabu hiyo mechi 393 na kupachika mabao 183 yanayomfanya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi wa muda wote wa klabu hiyo. Kitendo cha Mourinho kumtema katika kikosi chake, kilionyesha kama ndiyo utakuwa mwisho wake katika soka, lakini huenda ikawa ni kinyume, kwani si mara moja kocha huyo wa zamani wa Real Madrid amekuwa akifanya makosa ya kuwaacha wachezaji ambao baadaye hugeuka lulu wanakokwenda.

 

Lukaku mwenyewe, aliyemnunua kwa bei mbaya kutoka Everton, alimtema wakati akiwa Chelsea, alipomlazimisha kwenda kucheza kwa mkopo, wakati huo akimtegemea nyota wake Didier Drogba. Na tena, alifanya hivyo alipomruhusu kuondoka, akidai hana mipango naye, Juan Mata, aliporejea.

 

NA: OJUKU OBRAHAM| IJUMAA

Leave A Reply