The House of Favourite Newspapers

Kuwaona Yanga dhidi ya Mamelodi Kwa Mkapa Mzunguko ni Bure

0
Afisa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe.

Afisa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe wakati akizungumza na waandishi wa habari leo, Dar es Salaam amesema Mechi ya  Yanga dhidi ya Mamelodi Sundowns itachezwa majira ya saa tatu usiku March 30, 2024. Mamelodi wataingia nchini siku ya Tarehe 28 March 2024 majira ya saa moja kamili usiku”

Viongozi wa Klabu yetu hawana tamaa ya fedha, ndio maana tumepunguza na kuondoa tiketi ya mzunguko kwa lengo la kuhakikisha wengi waje Uwanjani. Tumeweka maslahi ya mpira wa Tanzania mbele. Mechi ya Mamelodi ni kubwa mno lakini kwa kuwa lengo sio fedha ni hamasa basi tunawasihi mashabiki kujitokeza kwa wingi. Kiasi cha fedha ambacho ungelipia tiketi ya mzunguko basi utatumia kama nauli ya usafiri wa kukufikisha uwanjani na baada ya mchezo wetu uweze kurudi nyumbani salama”

“Najua wachambuzi wengi na waandishi hawaipi nafasi Young Africans SC dhidi ya Mamelodi. Nina uhakika Wachezaji sita mpaka saba wanaweza kuanza kwenye kikosi cha Mamelodi. Tunaichukulia poa Young Africans SC kwa sababu tu inatokea Tanzania. Lakini hii Klabu ingekuwa ipo DR Congo ingesifiwa sana kuliko inavyosifiwa sasa.

Mwananchi usisikilize uchambuzi wa mchambuzi yoyote yule. Tusipotezwe kwenye dira yetu. Young Africans SC ikiamua jambo lake hatuwezi kufeli. Nina uhakika kwa zaidi ya asilimia 100 kuwa tunakwenda kushinda mchezo ujao. Mtu akikwambia Mamelodi ina wachezaji wazuri mwambie hata sisi tuna wachezaji bora kuliko wao.”-

“Uongozi wa Klabu umekubaliana kuweka mkakati wa kupeleka mashabiki Afrika Kusini kwenye mchezo wa marudiano. Kama tulivyofanya wakati wa mchezo wetu wa nusu fainali CAFCC dhidi ya Marumo, (kwao kama kwetu) season 2 inaanza na Bei ya kushiriki ni ile ile tshs 2000 tu.

Vile vile tumeaanda usafiri wa kwenda Afrika Kusini kwa njia ya basi, ambapo utahitaji kuwa na kiasi cha Tsh 600,000 gharama za kwenda na kurudi. Watu 10 kutoka Morogoro tayari wameshalipa, endelea kufuatilia mitandao yetu ya kijamii tutaweka utaratibu wa namna ya kulipia” amesema Ally Kamwe

Leave A Reply