The House of Favourite Newspapers

Mahafali Kidato cha Sita Yafaana Sengerema Sekondari!

0
Licha ya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya kidato cha sita mwaka 2023 kwa kufuta daraja la nne na sufuri shule ya Sekondari Sengerema inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vitabu vya sayansi na vifaa vya maabara  sambamba na vitabu vya masomo ya sanaa   hali inayopelekea walimu kutafuta vitabu vya ziada  sehemu mbalimbali kukabiliana na changamoto hiyo.
Matokeo ya kidato cha sita mwaka 2023 shule hiyo imefanya vizuri kwa kupata daraja la kwanza wanafunzi 408 ,daraja la pili wanafunzi 263, daraja la tatu wanafunzi watano huku ikifuta daraja la nne na daraja sufuri.
Hayo yamebainishwa  leo march 21,2024 kwenye  risala ya wahitimu wa kidato cha sita shule ya Sekondari  Sengereme ambapo inafanya  maafari ya 35 ya shule hiyo iyosomwa Jackison Myawa kwa niaba ya wanafunzi  wanaotarajia kufanya mtihani ya kuhitimu kidato cha sita.
Jackison amesema wanafunzi wanaotarajia kuhitimu kidato cha sita mwaka huu  ni wanafunzi 588 kati ya wanafunzi 590 wa kidato hicho
ameiomba  Serikali kumaliza changamoto hiyo ili iwarahishie walimu kufundisha na wanafunzi waweze kujipata vitabu vya kujisomea.
Akizungumuza kwa njia ya Simu mkurugenzi wa halmashauri ya Sengerema Binuru Shekidele amesema kutokana na upungufu wa vitabu mashuleni na vifaa vya maabara ofisi yake imejipanga kununua  vifaa hivyo ili kuondoa uhaba huo kwenye shule hiyo wanafunzi wapate namuna nzuri ya kujifunza ili wafaulu mitihani yao.
Shule Sekondari Sengereme yenye kidato cha tano na sita inaidadi ya walimu 50 na watushi Saba ambao siyo walimu pia inawanafunzi wapatao  1201 kidato ya tano na sita.
” Tunaiomba Serikali kumaliza changamoto zinazoikabili shule hii ili iendelee kufanya vizuri kwenye Matokeo yake ya kidato cha sita, amesema Miyawa.
Akisoma taarifa ya shule hiyo  kwenye  maafari ya 35 mkuu wa shule ya Sekondari Sengerema Zakaria Kahema kuwa shule hiyo imejipanga kuhakisha inafuta daraja la tatu ,nne na sufuri  ili iendeleea kufanya vizuri.
Hatua ya kufuta madaraja hayo inatakiwa kuondoa changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo ya upungufu wa vitabu vya sayansi na maabala sambamba na vitabu vya masomo ya Sanaa.
Mapungufu mengine ni kutokuwa na genereta ya kufua umeme wakati umeme unapokatika wanafunzi hushindwa  kijisomea upungufu wa mashine ya kudurufu mitihani kutokana na mazoezi kufanyika mara kwa mara tukikabiliana na changamoto hii itasaidia kufikia malengo yetu.
Kwa upande wake mgeni Rasmi katika maaafari hayo Yanga Makaga ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema na wadau mbalimbali wa maendeleo  wamejitolea kuhakisha wanapata genereta na mashine za kudurufu mitihani ili kukabiliana na changamoto hizo.
Wadau mbalimbali wa maendeleo wamejitolea kununua genereta na mashine za kudurufu mitihani kwenye shule ya Sekondari Sengerema kwa ajili ya kuongeza  ufaulu na kufuta daraja la tatu ,nne na sufuri.
Leave A Reply