The House of Favourite Newspapers

#Trending: Kwa Ahadi Ya 45,000/= Tzs, Alichokifanya Meek Mill Kwa Huyu Ombaomba Kitakufurahisha… (Video)

Maisha ni kupambana mdau, hakuna vitu vya bure siku hizi na hiyo sio kwa sisi wabongo tu bali hata kwa wenzetu walio mbele. Nimekutana na hii moja ya rapa kutoka Marekani Meek Mill itakayokufurahisha.

Weekend hii iliyoisha rapa kutoka Marekani Meek Mill alikuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya video inayomuonesha rapa huyo akimpigisha ombaomba pushups kwa ajili ya pesa kusambaa mitandaoni…Ilikuaje? Acha nikutonye!

Ombaomba huyo alimuomba Meek Mill na rafiki zake wamsaidie hela lakini badala ya kumpatia tuu, Meek Mill aliamua kumfanya ombaomba huyo aihangaike pesa hiyo kidogo.

Kupitia Insta LIVE feed yake Meek Mill alilirekodi tukio zima ambapo alisikika akisema;Nipe pushups kumi, alafu nitakupa $20 sasa hivi. Hatugawi hela za bure sisi…

Dola $20 ni sawa na Tzs. 45,000/= za Kitanzania kwa sasa na kwa kuwa yule ombaomba alikuwa hana jinsi na ana shida na pesa akainama chini na kuanza kuzipiga zile pushups 20 ili aweze kupewa pesa na sio tuu kuipata kirahisi rahisi.

Itazame video hiyo hapa chini, kisha niambie ingekuwa ni wewe kwa shillingi 45,000/= ungezipiga hizo pushups? Na je alichokifanya Meek Mill kwa huyu mzee unadhani ni sahihi?

 

IMEANDIKWA NA: Sandra Brown.

Comments are closed.