The House of Favourite Newspapers

Kwa Majonzi, Kabendera Amlilia Mama Yake, Asimulia Jela Kulivyo – Video

0

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imemuhukumu Mwandishi wa Habari za uchunguzi Erick Kabendera kulipa faini na fidia ya jumla ya Tsh. Milioni 273 baada ya kukiri makosa yaliyokuwa yakimkabili ya utakatishaji fedha na ukwepaji kodi huku akiondolewa shitaka la kuongoza genge la uhalifu.

 

Mahakama imetoa uamuzi huo jana Jumatatu, Februari 24, 2020, baada ya mwenendo wa kesi iliyokuwa ikimkabili inafuatia kukamilika kwa mazungumzo na makubaliano baina yake na Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP).

 

Kabendera amekiri shtaka la kukwepa kodi ya TZS milioni 173. Ameahidi kulipa kiasi hicho kwa mafungu ndani ya kipindi cha miezi 6. Kwa shtaka hilo, mahakama imeamuru alipe faini TZS 250,000 au kifungo cha miezi sita jela.

 

Kabendera amekiri pia shtaka la utakatishaji fedha na mahakama imeelezwa kuwa mwandishi huyo maarufu wa habari za kiuchunguzi, tayari ameshalipa kiasi cha TZS milioni 100 kama faini ya shtaka.

 

Baada ya kuachiwa huru, Kabendera amezungumzia kuhusu kifo cha mama yake huku pia akisimulia maisha aliyoyapitia mahabusu ambako amekaa kwa zaidi ya miezi saba.

 

MSIKIE KABENDERA

Leave A Reply