The House of Favourite Newspapers

Lady Gaga na Taylor Kinney watengana!

0

Taylor Kinney, left, and Lady Gaga arrive at the Oscars on Sunday, Feb. 28, 2016, at the Dolby Theatre in Los Angeles. (Photo by Jordan Strauss/Invision/AP)Marekani

Mwanamuziki na mwigizaji mashuhuri kutoka Marekani Lady Gaga amefichua kwamba yeye na mchumba wake “wametengana” kwa muda.

Hii imedhihiisha mara baada ya staa huyo kuandika ujumbe kwenye Instagram na kuwaomba mashabiki wawasaidie na kuwaunga mkono.

Lady Gaga na Taylor Kinney wamekuwa pamoja kwa miaka mitano lakini uvumi umekuwa ukienea kwamba urafiki wao umeingia kutu. Amesema bado wanapendana sana lakini juhudi zao za kutaka kutimiza ndoto zao maishani, kuwa mbali pamoja na shughuli nyingi za kikazi vimetatiza uhusiano wao.

Lady Gaga, 30, alianza mahusiano na Taylor Kinney, ambaye ni mwigizaji na mwanamitindo, baada ya kukutana naye akiandaa video ya wimbo wa You and I mwaka 2011, ndipo akamchumbia siku ya wapendanao mwaka 2015, na akamvika pete ya almasi ya umbo la moyo.

Wawili hao hawajapigwa picha sana wakiwa pamoja siku za karibuni. Gaga, ambaye jina lake halisi ni Stefani Joanne Angelina Germanotta, pia ameonekana mara kadha akiwa hajavalia pete ya uchumba.

Mashabiki wao huwaita wawili hao “Tayga”, kutokana na majina yao Taylor na Gaga. Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakishangaa kuhusu hatima ya mbwa wawili wanaomilikiwa na wawili hao, ambao majina yao ni Koji na Miss Asia Kinney.

Leave A Reply