The House of Favourite Newspapers

Ligi Kuu Simba siku 10 mechi 5

SIMBA ipo katika kipindi kigumu cha ratiba ya Ligi Kuu Bara, hiyo ni kutokana na kutakiwa kucheza mechi tano ndani ya siku kumi, ambapo kutokana na hali hiyo, takwimu zinaonyesha kuwa wakishinda mechi hizo zote watajiweka katika mazingira mazuri ya kubeba ubingwa.

 

Timu hiyo itacheza mechi hizo tano mfululizo kuanzia wikiendi hii, ikiwa ni baada ya kuifunga Coastal Union mabao 2-1, juzi Jumatano.

 

Simba ambayo ina pointi 60 kwa sasa, ina’ viporo’ tisa ili wafikie idadi sawa na mechi za Yanga ambao wamecheza mechi 32 na wanaongoza msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 74.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Katibu Mkuu wa Simba, Dk Anold Kashembe, alisema kocha wao pamoja na wachezaji wanatambua ugumu wa ratiba hiyo, hivyo wamejipanga kwenda kupambana katika mechi zote. “Ratiba hii tumekubaliana nayo, kocha pamoja na wachezaji wameikubali, ni lazima tupambane.

 

Mipango yetu tulishajadiliana kuwa ni vijana na kocha wakapambane na tuweze kuondoka na matokeo kwenye mechi hizo na kutetea ubingwa wetu tena. “Ratiba hii tulishirikishwa na bodi ya ligi, kwa jinsi hali ilivyo haikwepeki hata kidogo, kupambana ndiyo jambo la msingi.”

RATIBA YA SIMBA

Aprili 20 vs Kagera (Kaitaba)

Aprili 23 vs Alliance (Kirumba)

Aprili 25 vs KMC (Kirumba)

Aprili 27 vs Biashara (Karume)

Aprili 30 vs JKT (Taifa)

 

(STORI NA MARTHA MBOMA, GPL)

SPOTI HAUSI: Sababu Zilizowatoa SERENGETI BOYS Kwenye AFCON!

Comments are closed.