The House of Favourite Newspapers

Lil Ommy: Harmonize Nilimshangaa, Sifanyi Kazi za Muziki wa Diamond

0

HIVI Karibuni msanii Harmonize aliwahi kumtuhumu mtangazaji wa The Switch ya Wasafi Fm, Lil Ommy akidai ni moja ya watu wanaotumika kumchafua, jambo ambalo Lil Ommy amelikanusha hii leo kwenye moja ya Hafla ya Dstv.

 

Akijibu swali ambalo aliulizwa kama tuhuma hizo zina ukweli wowote, Lil Ommy amejibu kuwa; “Mwenyewe niliona surprise tu nakutana na hizo clip, nilichukulia kawaida ni mambo ya sanaa, unajua nimekuwepo kwenye industry kwa muda mrefu, so sipendi kuingilia vitu ambavyo vina mielekeo tofauti.

 

“Nadhani toka nimeingia Wasafi kuna baadhi ya watu wana matatizo yao wao na sijui kwenye vitu gani, unaweza kukuta mtu mwingine anakuingiza kwenye mambo ambayo wewe haupo.

 

“Kuwa Wasafi haimaanishi mimi nafanya kazi za muziki za Diamond, mimi sio Meneja wa Diamond, sihusiki na masuala ya muziki nahusika na Media. So inawezekana mwingine ana hizo hisia, lakini sina noma, sijawahi kuacha kucheza nyimbo zake (Harmonize), hata The Switch nyimbo zake tunacheza,” – Lil Ommy.

Leave A Reply