The House of Favourite Newspapers

Lissu Amaliza Matibabu, Asitisha Kurejea Tanzania – Video

ALIYEKUWA Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, ambaye alinusurika kuuawa miaka miwili iliyopota nyumbani kwake, Area D, Jijini Dodoma amesema amesitisha mpango wake wa kurudi nchini kwa sasa.

 

Akihojiwa na Kituo cha VOA – Swahili huko Washington, amesema kilichobaki kwa sasa ni viongozi wenzake waliopo Tanzania wamhakikishie kuwa Tanzania ni salama.

 

Amesema:  “Mazingira ya kiusalama si mazuri, wale walionipiga risasi 16 mchana kweupe katika nyumba za Serikali bado wanaitwa wasiojulikana. Pia kuna maneno yanajitokeza kwenye mitandao ya kijamii kuwa ngoja aje safari hii hatutakosea shabaha.”

 

Hapo awali, Lissu alisema akimaliza matibabu nchini Ubelgiji atarejea Tanzania siku ya tarehe 7 Septemba mwaka huu.

Comments are closed.