The House of Favourite Newspapers

VIDEO: WASAFI FESTIVAL KUZINDULIWA JULAI 12, MULEBA, BUKOBA

 

Mkurugenzi wa Wasafi Media, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’.

MKURUGENZI wa Wasafi Media, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) ametangaza leo Juni 25, 2019, kuzinduliwa rasmi kwa msimu wa pili wa Wasafi Festival 2019  ambapo shoo ya kwanza itafanyika katika Mkoa wa Bukoba Wilaya ya Muleba, Julai 12, 2019 mwezi ujao.

Diamond ameyasema hayo katikahotali ya  HyattRegency jijini Dar es Salaam akiongea na wanahabari

“Napenda Kutangaza rasmi kuwa Wasafi Festival 2019 nimeizindua na mkoa wa kwanza ambao tunaenda kuwasha moto wa burudani ni pande za Mulba na shoo itapigwa pale tarehe 12 mwezi wa saba.

“Tukimaliza tu Mulba, tunapunzika siku moja, kisha tarehe 14 Julai 2019 tunaingia Mkoa wa Tabora kuwasha moto.   Niwaambie tu mimi binafsi nimejipanga kisawasawa, na sina utani na steji.  

“Baada ya Muleba na Tabora tutaenda kwa ndugu zetu wa Iringa tarehe 20 Julai 2019 na huwa wanatupa upendo wa ajabu na msimu huu tunahakikisha Iringa hawatatusahau katika sekta ya burudani

“Msimu huu tutaufanya kitofauti aana, na nipende kuwashukuru BASATA (Baraza la Sanaa la Taifa) kwa kutupatia kibali kwa mara nyingine tena kuweza kufanya Tamasha la Wasafi Festival 2019” alisema Diamond.

 

Comments are closed.