The House of Favourite Newspapers

SADC: Magufuli Ataka Zimbabwe Iondolewe Vikwazo – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameziambia nchi za Magharibi waondoe vikwako vya uchumi kwa nchi ya Zimbabwe.

 

Akihutubia Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuia Kusini mwa Afrika –SADC mara baada ya kukabidhiwa Uenyekiti wa nchi wanachama wa Jumuiya Kusini mwa Afrika na Rais wa Namibia Mhe Dkt Hage Geingob leo Jijini Dar-es-salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano waJulius Nyerere.

 

Rais Magufuli amesema kuwa sababu zilizosababisha nchi ya ndugu zangu, kaka zangu na dada zangu wa Zimbabwe kuwekewa vikwazo havipo tena. Hivyo ni vema Jumuia ya Kimataifa ikaondoa vikwazo hivyo kwani vinawaumiza watu wasio na hatia.

 

Rais Magufuli amesema “Naomba ndugu zangu wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika -SADC tuungane na kupaza sauti zetu,tuwe na kauli moja, kutamke kwa pamoja sasa vikwazo Zimbabwe basi”.

 

Akielezea hali halisi ya uchumi na pato la Taifa moja moja kwa upande wa nchi wanachama Rais Magufuli amesema kuwa sababu kubwa inayotufanya tuwe na uchumi dumavu usiokuwa ni kwa sababu ya kuendelea kutegemea kuuza malighafi kwa nchi zilizoendelea.

 

“Ukiuza malighafi ujue unauza na nafasi za ajira za watu wako, ndio maana kwetu Barani Afrika na hususan Kusini mwa Jangwa la Sahara tuna tatizo kubwa kwa vijana wetu kupata ajira ”.

Rais Magufuli ameongeza kwa kusema utatuzi wa jambo hili ni kuamua SADC kuwa nchi za Viwanda, kwa kuwa hakuna nchi yeyote duniani ambayo imeendelea bila kuwa na Viwanda.

 

Maana wanahakikisha wanaongeza thamani bidhaa zao na kwa kuwa gharama ya uzalishaji ni ndogo hata tufanye vipi hatutaweza kushindana nao mpaka pale tutakapoamua kuwa nchi za Viwanda.

 

Hivyo basi ajenda yangu kubwa kama Mwenyekiti wa SADC ni kuwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, ambayo itajikita na kuwekeza kwenye Viwanda. Hii itatupa nafasi ya kutimiza malengo yetu kama inavyosema kauli mbiu yetu ya Mazingira Wezeshi kwa Maendeleo Jumuishi na Endelevu ya Viwanda, Ongezeko la Biashara na Ajira Kikanda.

 

Akitolea baadhi ya mifano ya hali halisi ya ukuaji wa uchumi Rais Magufuli amesema kuanzia mwaka 2015 pato la Taifa katika nchi wananchama imekuwa kwa asilimia 16 hadi kufikia 17 kwa mwaka 2018 katika nchi wanachama wa SADC.

 

Akielezea uzoefu alioupata mara baada ya kuamua kufanya ziara katika nchi wananchama wa SADC, Rais Magufuli amesema Nimegundua nchi nyingi zinaupungufu wa chakula, kwa kuwa hazikupata mvua za kutosha kwa ajili ya kulima mazao ya chakula. Hii imesababisha baadhi ya nchi kuwa na ukame ulioleta njaa, pamoja mafuriko, na maafa ya kimbunga.

 

Akitaja visababishi vya kushindwa kushirikiana ndani ya nchi wananchama na kusababisha biashara kudorora Rais Magufuli amefafanua kuwa ni Ukosefu wa taarifa katika nchi wanachama, akitolea mfano jambo amesema Tanzania imevuna vyakula vingi na kupata mazao ya ziada lakini nchi za SADC, hazina taarifa na inashangaza wanahangaika kuagiza chakula kutoka nchi za mbnbali na wakati hapa Tanzania chakula kipo.

 

Lakini changamoto nyingine ni kutokuwa na miundombinu rafiki ambayo nchi wanachama wanaweza kuitumia kusafirisha chakula kutoka nchi moja kwenda nyingine. Jambo hili la miundombinu tulifanyie kazi ili tuweze kupubguza gharama ya usafirishaji, pia kusafirisha kwa muda mrefu.

 

Changamoto ya tatu ambayo inatufanya tusipate masoko ya nje ni ubora na viwango vya bidhaam zetu kutokidhi viwango vya Kimataifa. Hivyo ni vema tukaamua kufanya biashara sisi wenyewe maana tutaweka ubora na viwangu vyetu na kuhimizana polepole hadi kuvikia viwango vya Kimataifa.

 

Tuchangamkie kuweka sheria taratibu na miongozo ambayo itatunufaisha sisis wananchama kufanya biashara wenyewe kwa wenyewe na kuondoa vikwazo vya biashara ndani na nje ya nchi zetu ili nchi wanachama waweze kufanya biashara kwa pamoja hapa ndio tutakuza uchumi wetu.

 

Aidha, eneo la nchi za SADC ni eneo lenye utulivu na amani kuliko maeneo mengine ya kikanda ambayo yamegubikwa na vita na madhila ya wananchi ya hapa na pale. Ambapo amani na utulivu ni muhimu katika suala zima la kukuiza uchumi.

 

Pia utulivu huu unaletwa na hali ya ukomavu wa demokrasia katika kanda hii ambayo katika historia kwa mara ya kwanza Taifa la Jamhuri ya Watu wa Kongo –DRC wameweza kufanya uchaguzi kwa uhuru naamani na kumpata Rais ambaye amechaguliwa kidemokrasia mwaka 2018.

 

Akinukuu usemi wa Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe Rais Magufuli amesema “Never never ever give up in peace and security for this region” yaani “Msikubali msikubali kamwe kukata tama linapokuwa suala la amani na utulinukatia kanda hii” Amesisitiza Rais Magufuli.

 

Naye Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Rais wa Jamhuri ya NamibiaMhe. Dkt Hage Gein amesema kuwa ni lazima nchi wananchama kuhakikisha wanatekeleza Mkakati wa SADC wa kuwa na biashara hurubila vikwazo katika mipaka yetu. Pia kuhakikisha tunakuwa na usalama wa chakula.

 

Aidha, Nchi wanachama kuwa na Mpango maalum wa kudhibiti maafa na majanga yanapotokea na kuhakikisha nchi wanachama wanakuwa na uwezo wa kuzisaidia nchi zilizoadhirika kwa njia moja au nyingine ikiwa pamoja na Jumuiya ya Kimataifa.

 

Ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi ni vena tukahakikisha tunaacha kukata miti hovyo na Juhudi zifanyike kila nchi mwananchama kuhakikisha tunakuwa na vyanzo vya nishati vinavyokubalika na kulinda mazingira ili kuokoa uchafuzi wa mazingira.

 

Akimalizia amesisitiza ukuzaji wa uchumi kwa nchi wananchama kwa kuhakikisha Serikali kuhamasisha sekta binafsi kuanzisha viwanda vya madawa, vitendanishi na vifaa tiba, kuongeza dhamani mazao yetu na kushawishi sekta binafsi kuwekeza katika Viwanda na kuwawekea mazingira wezeshi ili wazalishe.

 

Naye Rais wa Jamhuri ya Watu wa Madagascar Mhe. Andry Nirina Rajoelina amesema nazishukuru nchi za SADC kwa kufanikisha nchi yangu kuwa kwenye usalama na utulivu. Pia, tunashukuru kwa nchi wananchama kusimamia uchaguzi mkuu wa kwetu salama.

 

Akielezea ushirikiano wa SADC na mashirika ya fedha Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt. Akinwumi Adesina amesema nchi zote za SADC zimefaidika kwa njia moja au nyingine katika kuipatia fedha miradi mbalimbali ya maendeleo.

 

Hivyo naomba tendelee kushiriiabana zaidi ili kufanikisha malengo ya maendeleo katika nchi wanachama. Aidha, uhusiano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika na SADC uendelee kuimarika katika kuhakikisha wananchi wa nchi husika wanafaidika na fedha zinazotolewa.

FUATILIA MKUTANO HUO HAPA

Comments are closed.