The House of Favourite Newspapers

LIVE: Mwili wa Mngereza wa BASATA Waagwa Karimjee

0

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa, amewaongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza, aliyefariki Desemba 24, 2020, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alipokuwa anapatiwa matibabu, anaripoti Eleuteri Mangi, WHUSM-Dar es Salaam.

 

Tukio hilo limefanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo Jumanne, Desemba 29, 2020, ambapo kulikuwa na ibada fupi ya kumuombea, salamu za rambirambi pamoja na nyimbo maalum kutoka kwa wasanii na vikundi vya sanaa walioimba nyimbo za maombollezo kumsindikiza kiongozi huyo.

 

Pamoja na Bashungwa, walikuwapo pia viongozi mbalimbali wa serikali, familia, watumishi wa wizara na  BASATA, wasanii, wadau wa tasnia ya sanaa, ndugu, jamaa na marafiki ambapo baadaye safari ya kuelekea Suji wilaya ya Same Mkoa wa Kilimanjaro ilianza ambapo mwili wa mrehemu utazikwa kesho Jumatano, Desemba 30, 2020.

 

Mngereza atakumbukwa kwa umahiri wake mkubwa wa kuisimamia sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya mwaka 1984 na kanuni zake na uwezo wake wa kusimia maadili katika kazi za sanaa pamoja na kuifahamu sekta kwa mapana yake, hatua iliyosaidia kukuza maendeleo na utengenezaji wa kazi za sanaa nchini zenye kujali ubora na maadili.

 

Leave A Reply