The House of Favourite Newspapers

Prof. Mkumbo na Mikakati ya Kuboresha Miundombinu ya Maji, Dar na Pwani

0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo amesema wizara yake imeahidi kuboresha huduma ya maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Amesisitiza kwamba huo ndiyo wito na changamoto kubwa kwa wafanyakazi wa wizara yake ambao wataendesha huduma hiyo kwa msingi wa biashara kwa maana ya kutoa huduma na kutengeneza faida kwa ajili ya kuendeleza huduma hiyo.

Alifafanua kwamba hilo litafanyika kuhakikisha kwamba huduma za maji zinawafikia wananchi katika sura ya huduma bora bila ya wao kujali wizara yake inaingiza kiasi gani cha pesa.

Leave A Reply