The House of Favourite Newspapers

KEVIN HART; KUTOKA UIGIZAJI HADI RIADHA!

0

MUIGIZAJI mahiri na aliyejizolea umaarufu mkubwa nchini Marekani kutokana na vichekesho vyake, Kevin Hart, ameweka wazi kuwa anatarajia kushiriki katika mashindano ya mbio za Marathon mwaka huu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameposti video inayomuonyesha akiwa mafunzoni akijiandaa kwa ajili ya kukimbia umbali wa km 41 na video hiyo imeambatana na maneno yafuatayo:

“Wakati mwingine unatakiwa kuwaza na kuwa na malengo ya mbali zaidi, hata kama yanaogopesha. Nitashiriki katika mbio za Marathon nchini Marekani, hiyo ndiyo ndoto yangu na wewe je ndoto yako ni ipi?”
Mpaka sasa ameshamudu kukimbia umbali wa km 14, akiwa bado anaendelea na mafunzo kwa ajili ya kupata uzoefu zaidi na hatimaye aweze kukimbia umbali unaotakiwa wa km 41.
Kevin Hart mwenye umri wa miaka 38 ambaye mbali na kuwa muigizaji aliyetamba kwenye filamu kama Think Like A Man, Grudge Match, Ride Along na nyingine nyingi, pia ni mwandishi wa stori na mtayarishaji wa filamu.
NA ISRI MOHAMED/GPL

Leave A Reply