The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli Ashuhudia Utiaji Saini Ujenzi Daraja la Salander -VIDEO

Rais John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Korea Lee Nak-yeon leo wanashuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa daraja jipya la Selander jijini Dar na njia zake.

 

Hafla ya utiaji saini wa mkataba huo inafanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo serikali kupitia wakala wa barabara Tanzania (Tanroads) inatiliana saini na mkandarasi aliyeshinda zabuni ya ujenzi wa daraja hilo. Daraja la Salander litaunganisha eneo la Aga Khan katika barabara ya Barack Obama na eneo la Coco Beach Katika Makutano ya baabara za Kenyatta na Toure.

 

“Daraja hili la Salender litapitisha zaidi ya magari ya 5o,000 kwa siku, hii itapunguza msongamano wa magari kwa jiji la Dar es Salaam. Nimemwomba Waziri Mkuu wa Korea, watusaidie kujenga daraja jingine kama hili pale Kigongo Ferry na Kamanga Ferry, ziwa Victoria jijini Mwanza. Hili litakuwa na urefu wa zaidi ya kilomita 3.

“Katika mkataba wake, ujenzi wa daraja hili la Salender utakamilika ndani ya miezi 36, nitashangaa kwa mkandarasi huyu mkubwa kutoka Korea akamaliza miezi yote hiyo na daraja hajamaliza, pesa ipo, site ipo na watu wa kufanya nkazi wapo.

 

“Baada hili tutaanza ujenzi wa meli kubwa Ziwa Victoria ambayo tuko kwenye hatua za mwisho kumpata mkandarasi, inavyoelekea anaweza kuwa ni Mkorea. Pia tutajenga meli nyingine Ziwa Tanganyika, yote haya tunaenda nayo kwa mpigo.

 

“Tunawashukuru Korea kwa ushirikiano wao na kutusaidia, nimemwomba Waziri wao Mkuu watusaidie soft loans (mikopo yenye masharti nafuu), yote haya tunayafanya ili kuibadilisha Tanzania iwe ya kisasa. Korea wametuunga mkono katika miradi mingi kuanzia hili na Malagarasi na Hospitali ya Mloganzila”, amesema Rais Magufuli.

 

Comments are closed.