The House of Favourite Newspapers

LIVE: Rais Magufuli Awatunuku Waliofanya Uchunguzi wa Makinikia

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Oktoba, 2017 amewatunuku vyeti wajumbe wa kamati zilizofanya uchunguzi wa kiwango, aina na thamani ya madini katika makinikia na baadaye kufanya mazungumzo na kampuni ya Barrick Gold.

LIVE: Rais Magufuli Awatunuku Waliofanya Uchunguzi wa Makinikia

 

Tanzania na Barrick Gold Corporation zilifikia makubaliano tarehe 19 Oktoba, 2017 na kutiliana saini mkataba wa kutekeleza mwelekeo mpya wa namna kampuni hiyo itakavyoendesha biashara ya madini ya dhahabu yanayochimbwa katika migodi yake hapa nchini, pamoja na kulipa takribani Dola za Marekani milion 300 za kuonesha nia njema ya kufidia madai ya upotevu wa mapato yaliyotokana na biashara hiyo na Kampuni ya Madini ya Barrick Gold Corporation.

Akizungumza ikulu leo, Rais Magufuli alisema Watanzania aliowatunuku vyeti vya heshima, wamefanya kazi kubwa sana ya kusimamia rasilimali za taifa, na kusisitiza kwamba haikuwa kazi rahisi kukamilisha kazi hiyo ya hatari.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android Bofya ===> Google Play

iOS Bofya ===>Apple Store

Leave A Reply