The House of Favourite Newspapers

Video: Simba Wanafanya Mkutano Dar, Malengo Kutwaa Mataji

0

MIRTAZA Mangungu, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kuhakikisha kwamba wanashinda mataji.

Simba ni mabingwa watetezi wa ligi wakiwa nafasi ya pili na pointi 14 huku Yanga wakiwa ni vinara wa ligi na wana pointi 16.

Maneno hayo ameyasema katika mkutano mkuu wa Wanachama wa Simba ambao unafanyika leo Novemba 21 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikitano wa Julius Nyerere.

“Kama ilivyo nalengo ya Simba ni kuhakikisja tunashinda mataji. Naomba tuendelee kushirikiana ili tufanikishe jambo hili,”.

Kabla ya Wanachama kuingia kwenye mkutano wa leo walikuwa wanahakikiwa kadi zao pamoja na suala la kulipia ada ya uanachama.

“Kipekee tutoe shukrani za kipekee kwa Mwenyekiti wa Bodi aliyepita, Mohammed Dewji kwa namna alivyojitoa. Chini ya uongozi wake tumeshinda makombe manne mfululizo ya ubingwa wa Ligi Kuu. Tunamshukuru sana.”

“Malengo yetu msimu huu ni kutetea ubingwa, kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa lakini tumeteleza lakini Mwenyezi Mungu ametupa nafasi kwenye Kombe la Shirikisho. Kipaumbele namba moja amepewa mwalimu ni kufika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho na kutetea ubingwa wa Ligi Kuu. Mashindano yote ambayo tunashiriki tunataka kushinda.” amesema CEO Barbara Gonzalez

Leave A Reply