The House of Favourite Newspapers

JPM Azindua Daraja la Furahisha, Akumbuka Alivyobomoa Nyumba Yake – Video

0
Daraja la Furahisha, Ilemela, Mwanza.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumatatu, Oktoba 30, 2017 ameanza ziara yake ya siku mbili jijini Mwanza na kuzindua Daraja la Waenda kwa Miguu la Furahisha, lililopo wilayani Ilemela mkoani humo ambapo pia atazindua Kiwanda cha dawa za binadamu na kiwanda cha plastiki.

Katika uzinduzi huo ambao Rais aliongozana na mkewe, Mama Janeth Magufuli, pia viongozi mbalimbali wa serikali walihudhuria akiwemo mwenyeji wake, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bwana John Mongella, Waziri wa Viwanda Mhe. Charles Mwijage, Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula na wengine.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais amewataka wananchi wa Mwanza walitunze daraja hilo kwani ni kichocheo kikubwa cha ukuaji uchumi na kupunguza ajali zilizokuwa zikitokea eneo hilo kipindi cha nyuma.

“Ndugu zangu nasema leo nina furaha kama jina la daraja kwa sababu mimi natambua historia ya eneo hili. Eneo hili lilikuwa linatambulika kama blackspot kwa sababu ya ajali nyingi sana kutokea hapa. Wakati naomba kura nilisema nitatengeneza daraja la Furahisha. Wananchi mkasema haiwezekani, nikasema itawezekana, nashukuru wananchi wa Mwanza kwa kutuamini. Niwaombe watu wa Mwanza mlinde daraja hili msipitishe pikipiki pale.

“Nilivyokuwa waziri wa ujenzi kwa kushirikiana na Mkuu wa mkoa tulivunja nyumba ili kutanua barabara, leo naona mmevunja nyumba ya Madaraka, Hongereni sana maana ilikuwa sehemu ya wazi. Pia hongereni kwa kuvunja nyumba ya CCM amabayo ilikuwa kwenye sehemu ya road reserve. Na mimi nilijivunjia ukuta wa nyumba yangu pale Solomoni Nassor. Wakaandika waziri ajivunjia ukuta

“Nilipozuia sherehe za Mapinduzi watu walisema sipendi hata mapinduzi lakini nikasema mimi ni Rais na nimeamua kutuma fedha hizo kutengeneza Mwanza na zile za uhuru zilijenga Dar es Salaam. Inaweza tokea sherehe nyingine nikasema fedha hizo zikajenge sehemu nyingine

“Sidhani kama kuna daraja kama hili sehemu yoyote ya Tanzania, daraja linajiwasha tu taa lenyewe na ndugu zangu wa Mwanza mtafungia ndoa hapo. Ndugu zangu naomba mlitunze daraja hili, kwanza linaonyesha picha ya samaki hata aliyetengeneza daraja hili anakula samaki,” alisema Magufuli.

“Mbali ya kuendeleza sekta ya usafirishaji wana Mwanza mnafahamu kuwa tunajenga reli ya standard Gauge inayotoka Dar kuja Mwanza itaenda Rwanda mpaka Burundi Mpaka Kigoma. Tunaijenga kwa fedha zetu bila kukopa.

“Daraja la Busisi hadi Kigongo usanifu umeshaanza, utengenezaji unawezekana. Kila kitu kipya huwa ni miujiza hata niliposema mtu anaweza kutoka Mtwara mpaka Mwanza kwa kutumia lami watu walidhani nimuujiza ila leo imewezekana

“Hawa watu wa Kidoto na Muhonze ndio wamenipa urais na kwa vile serikali yangu ina huruma na kwa vile kuna sheria inasema ardhi ipo chini ya uangalizi wa rais nasema wasiwabomoleshe kwanza. Waziri wa ardhi na viongozi wa chama (CCM) na wakuu wa mikoa mkae wiki ijayo mtoe mapendekezo. Yapo maeneo ambayo lazima watu wahame kama wale amabo wapo ndani ya airport,” alieleza Rais Magufuli.

Daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha ambalo rais Magufuli ameifungua leo liligharimu fedha kiasi cha shilingi bilioni 4.747, limetengenezwa na Watanzania na linaweza kupitisha watu 60 kwa wakati mmoja ambalo lilianza kujengwa mwaka jana 2016.

Leave A Reply