The House of Favourite Newspapers

Lori la Mafuta Lagonga Mti na Kupinduka Shinyanga

0

WATU wawili wamejeruhiwa baada ya Lori la mafuta gari lenye namba za usajili T674 BAA aina Tanker lenye tela lenye namba za usajili T260 BLA kugonga mti na kupinduka katika eneo la Ugweto kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga barabara kuu ya kutoka Shinyanga kwenda Mwanza.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba ambaye amefika eneo ajali ilipotokea amesema ajali hiyo imetokea leo Ijumaa Agosti 21,2020 majira ya saa 11 na dakika 45 asubuhi.

 

 

“Ajali hii imetokea leo lori hilo likiendeshwa na Yusto Elinaja (51) mkazi wa Dar es salaam likitokea Dar es salaam kuelekea Mwanza lilipofika eneo la Ugweto dereva alikuwa anajaribu kupita gari jingine ‘Over take’ lililokuwa mbele yake lenye namba za usajili T440 BWJ Scania ndipo Dereva aliligonga gari jingine kwa nyuma na kuacha barabara na kugonga mti na gari hilo kupinduka”, amesema Kamanda Magiligimba.

 

 

Amesema Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa lori ambapo alijaribu ku overtake bila kuchukua tahadhari.

 

 

“Katika ajali hiyo watu wawili wamepata majeraha na wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Dereva wa gari hilo amepata maumivu ya mkono wa kulia,mwingine ni Elinaja ambaye amevunjika mkono wa kushoto na mguu wa kulia na Magari yote mawili yamepata uharibifu mkubwa”, ameeleza Kamanda Magiligimba.

 

Aidha, amewakata madereva kuongeza umakini wanapoendesha vyombo vya moto na kuzingatia sheria barabarani.

 

 

Kufuatia ajali hiyo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga likiongozwa na Kamanda wa Polisi mkoa ACP Debora Magilimba walifika kwa wakati eneo la ajali hiyo na kufanikiwa kudhibiti vitendo vya wananchi kusogolea gari hilo la mafuta ili kuepuka vitendo vya wizi wa mafuta na vifaa vya gari kuepuka madhara zaidi.

 

 

Pia Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiongozwa na Afisa Operesheni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga Inspekta Edward Lukuba wamefika mapema eneo la tukio.

Leave A Reply