The House of Favourite Newspapers

Lugola Amkabidhi Ofisi Simbachawene – Video

0

ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ambaye ni Mbunge wa Mwibara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amekabidhi rasmi Ofisi ya Wizara hiyo kwa Waziri mpya aliyeteuliwa hivi karibuni, George Simbachawene katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, jana Januari 30, 2020.

 

”Waziri nakufahamu, Rais amekuamini kuongoza Wizara hii, hakubahatisha. Anatambua uwezo uliokuwa nao. Nilipokabidhiwa Wizara hii, ni Wizara ambayo kwa muda mrefu ina changamoto nyingi; changamoto ya uhaba wa rasilimali watu kwenye vyombo vya ulinzi na usalama, changamoto ya majengo,” amesema Kangi Lugola.

 

Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amewataka watendaji wakuu wa Wizara yake kufanya kazi kwa ushirikiano kwa kuwa Wizara hiyo ina mambo mengi yayonahusiana na jamii.

 

Akizungumza katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo jijini Dodoma, baada ya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola, amewataka watendaji hao, kipindi hiki anajiandaa kuja mbele yao kuonyesha mbinu zake za utendaji kazi, wafanye kazi usiku na mchana, kwa yale yanayohitaji kufanyiwa kazi ili yaweze kufanyiwa kazi.

 

Leave A Reply