The House of Favourite Newspapers

Luizi: Griezmann Aliitumia Man U Kupiga Dili

0
Antoine Griezmann.

MCHEZAJI wa Atletico Madrid, Filipe Luis, amesema anaamini mchezaji mwenzake, Antoine Griezmann, aliwababaisha Manchester United ili wamthamini zaidi na hivyo kumpa mkataba bora zaidi.

Mlinzi huyo mahiri wa Atletico aliongeza kwamba Griezmann, mwanasoka wa kimataifa wa Ufaransa kweli anapenda kucheza katika Ligi ya Hispania (La Liga) lakini kwa kilichofanyika ni kwamba itachukua muda kabla ya kujiunga nayo.

Griezmann alikuwa chaguo namba moja la kocha Jose Mourinho wa Man U ili ajiunge nao msimu huu, lakini kupigwa marufuku kwa Atletico kusajili wachezaji, kulivuruga jambo hilo.

Tatizo pia lilikuwa kwa kocha Diego Simeone kupata nafasi ya kuziba nafasi ya mshambuliaji aliyekuwa naye iwapo angejiunga na Ligi Kuu ya Uingereza ambapo Griezmann alikuwa hataki kuondoka kwenye klabu hiyo bila ya mtu wa kusaidiana naye uwanjani.

Luis ambaye aliwahi kuwa mlinzi wa klabu ya Chelsea, alisema Griezmann aliitumia fursa ya kutakiwa na Atletico ili kujipandisha thamani katika Man U.

“(Griezmann) ni jamaa anayesema kweli,” Luis aliliambia gazeti la El Mundo na kuongeza: “Wachezaji kila mara huzungumza wanapohisi wamesahaulika. Hapo ndipo hukumbukwa na hupata fursa mbalimbali kutoka timu nyingi.

“Hivyo ataendelea kuchezea timu yake kwa muda mrefu ambapo mashabiki zake wafahamu hilo na aendelee kufunga magoli ambayo ndiyo tiba ya kila kitu.”

Spoti Hausi LIVE: Haruna Niyonzima Afichua Alivyotoka Yanga Kwenda Simba

Leave A Reply