The House of Favourite Newspapers

Lukuvi Atumbua Mtu Iringa – Video

0

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi,  amemwondoa katika nafasi yake  Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Wilbert Mtongani,  baada ya kubaini amefungua ofisi yake binafsi ambayo inashughulikia masuala ya ardhi, kiasi cha kumfanya apoteze muda mwingi wa kazi katika ofisi hiyo na kuisababishia halmashauri hiyo kukosa mapato yake.

 

Akiongea katika mkutano wa hadhara ambao lengo lake ni kupokea kero za ardhi katika mkoa wa Iringa, Lukuvi amesema amelazimika kuchukua hatua hiyo baada ya kuona mtumishi huyo anachukua muda wote wa kazi katika ofisi yake binafsi na kuwatoza wananchi kiasi kikubwa cha pesa kwa kushughulikia matatizo yao ya ardhi,  jambo ambalo limekuwa likiikosesha manispaa hiyo maduhuli yake halali.

 

Awali akimkaribisha Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi, amesema ofisi yake kwa kushirikiana na wataalamu imekuwa na utaratibu wa kudumu wa kushughulikia migogoro ya ardhi.

 

Leave A Reply