Lulu Diva: Nilimpenda Zaidi Lavalava Kuliko Mavoko, Adai Hamuogopi Mtu

Luludiva

UNAWEZA kuwa unajiuliza mbona watu wengi hawamo kwenye uhusiano wa kimapenzi au walikata tamaa baada ya kuwa kwenye uhusiano wa kwanza.

 

Jibu ni kuwa wengi walivunjika moyo kwani walikuwa wamewapenda wenzi wao kwa moyo wao wote lakini wenzi wao hawakuyaona hayo waliishia kuwasaliti.

 

Siyo kisa kimoja au viwili bali tumewaona watu mashuhuri, wasanii wa muziki na waigizaji wakipendana na baada ya muda wanaachana, huku wakitupiana maneno ya kashfa.

 

 

Nini hasa kinakosekana kwenye uhusiao wa kimapenzi katika karne hii ya sasa?

 

Ni wengi ambao wamekwa wakijiuliza haya, huku asilimia kubwa ikisema kwamba tatizo ni kukosekana kwa uaminifu; ndoa na uhusiano bila uaminifu siyo uhusiano tena.

 

Kwa upande wake, msanii wa muziki wa Bongo Fleva na Bongo Movies, Lulu Diva ameweka wazi ni ex yupi alikuwa anampenda zaidi kuliko mwingine.

Luludiva amesema alikuwa anampenda sana Lavalava kuliko Rich Mavoko

Lulu Diva anakiri kwamba, alimpenda zaidi msanii wa Bongo Fleva aliye chini ya Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Lavalava.

 

“Kati ya Rich Mavoko na Lavalava ulimpenda nani zaidi?” Lulu ameulizwa.

 

“Nilimpenda sana Lavalava,” Lulu Diva amejibu kwa ujasiri.

 

Lulu Diva ameweka wazi kwamba, haogopi mtu yeyote kwa chochote anachofanya maishani mwake;

 

“Siogopi mtu wala kitu! Sababu nikikosa mkate kwa kuona aibu hakuna atakaeniletea mkate mezani, kinywa changu kinausubiri mkono uufikie, basi siwezi kusubiri hadi watu waniamulie… Huyu ndiye mimi…”

CC; @sifaelpaul3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment