The House of Favourite Newspapers

Lusinde: Samia ni Magufuli, Wasimchafue Marehemu – Video

0

 

Mbunge wa Jimbo la Mvumi Livingstone Lusinde amesema kamwe Amani na Utulivu kwa watanzania hauwezi kuwepo kama kuna baadhi ya watanzania wanamsema Vibaya aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya Tano Hayati John Pombe Magufuli.

 

 

Lusinde amesema watu wanaomsema Vibaya Hayati Rais Magufuli leo ipo siku watamsema Vibaya Rais wa Tanzania Samia Suluhu kwa kuwa hiyo ni tabia.

 

 

“Leo Magufuli (Hayati Magufuli) anasemwe vibaya na sisi tupo hata 40 haijafika, hili jambo halikubaliki, hawa watu washike adabu na adabu ziwashike. Hatutaki warudie tena mambo ya kipuuzi kama hayo.

 

 

“Labda kuna wengine wanafikiri Samia alikuwa Benchi akaingia kucheza mpira hapana, Samia alikuwa anacheza pamoja na Magufuli, tunataka Watu wamheshimu, hauwezi kuondoa legacy ya Magufuli kwenye Nchi hii na Bara la Afrika, haiwezekani, hatuwezi kuwavumilia wanaomsema hayati Magufuli.

 

 

“Hawahawa wanaomsema vibaya leo Magufuli, watamsema vibaya Rais Samia. Kuna wanofikiri labda Rais Samia alikuwa benchi akaingia kucheza, hapana. Rais Samia alikuwa anacheza pamoja na Magufuli na aliyemtaja Samia ni Magufuli mwenyewe na alijua akiondoka yupo Samia.

 

 

“Tunataka watu wamheshimu Magufuli, huwezi kuondoa Legacy yake kwa nchi hii na Afrika. Kuna Mbunge gani hakutetewa na Magufuli? tuko humu ndani sababu ya Magufuli na Samia walipita kila sehemu wakisema tupeni huyu tutafanya nae kazi, sababu yao watu wakachaguliwa.

 

 

“Kuna watu walikuwa hawachaguliki hapa, lakini Hayati Dk John Magufuli na Mama Suluhu Samia walipita huko na kusema tuleteeni huyu, tutamrekebisha na tutafanya naye kazi, kwa sababu yao wakachaguliwa, leo hata arobaini bado wanamsema vibaya?” amesema Mbunge Lusinde.

 

Leave A Reply