Lwandamina Awamwagia Sifa Wachezaji Azam FC

BAADA ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Namungo, juzi Jumatatu, Kocha Mkuu wa Azam FC, George Lwandamina amewasifi a wachezaji wake na kusema kuwa wamecheza kwa kujituma.

 

Katika mchezo huo, mabao ya Azam yalifungwa na Iddy Nado dakika ya 19 na 73, huku ya Namungo yakifungwa na Edward Manyama dakika ya 24 naStephen Sey (DK 90).

 

Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ulipigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Azam wanashika nafasi ya tatu baada ya kukusanya pointi 28, huku Namungo wakiwa nafasi ya 13 baada ya kuvuna pointi 17.

 

Akizungumza na Championi Jumatano,Lwandamina alisema kuwa: “Ni matokeo ya mpira, timu imefanya vizuri kwani wachezaji walicheza kwa kujituma licha ya kupata sare.“

Utimamu wa wachezaji ni tatizo lililopo japo tupo katikati ya msimu na siyo ‘pre season’ kwa hiyo nitajitahidi wawe na utimamu, ili kuhakikisha wanapata matokeo kwenye michezo inayokuja.”Tecno


Toa comment