The House of Favourite Newspapers

Jengua Aswaliwa Mkuranga, Kuzikwa Mburahati Dar

0
Waombolezaji wakiswalia mwili wa marehemu Jengua nyumbani kwa mwanaye Mkuranga, Pwani  kabla ya kusafirishwa kuelekea nyumbani kwake Dar es Salaam ambapo maziko yanatarajiwa kufanyika leo Mburahati.

 

MWILI wa muigizaji nguli nchini Tanzania, Mohamed Fungafunga, maarufu kama Jengua unaswaliwa leo Desemba 16, 2020 nyumbani kwa mwanaye Mkuranga, Pwani kabla ya kusafirishwa kwenda  jijini Dar es Salaam.

Jengua alifariki asubuhi ya Desemba 15, 2020 nyumbani kwa mtoto wake Mkuranga.

Msanii huyo alipata umaarufu mkubwa katika mchezo wa runinga wa Kidedea uliokuwa ukirushwa na Kituo cha ITV na kutayarishwa na Chemchem Arts Group, akiigiza kama mzee katili na mwenye roho mbaya.

Enzi za uhai wake, Jengua aliigiza maigizo kama vile Kidedea, Handsome wa Kijiji, Kashinde na zingine nyingi.

 

PICHA NA IMELDA MTEMA

Leave A Reply