The House of Favourite Newspapers

Maafa Mafuriko China

0

MIJI mitano mikubwa katika jimbo la katikati mwa China, Hubei, imetangaza hali ya hatari baada ya mvua kubwa kukatiza huduma ya umeme na kubomoa nyumba kadhaa na kupelekea Watu wapatao 6,000 kuhamishwa.

 

Kwa mujibu wa Wizara ya Usimamizi wa Hali ya Dharura ya China, baadhi ya Miji kwenye Jimbo hilo ilikumbwa na mvua yenye ujazo wa hadi milimita 400 jana Alhamisi.

 

Shirika la Habari la China News Service linasema zaidi ya Mabwawa 770 ya kuhifadhia maji yalipindukia ujazo wake wa kawaida. Hali mbaya ya hewa kwenye Jimbo hilo imeshabomoa zaidi ya nyumba 3,600 na hekta 8,110 za mazao ya chakula na biashara.

 

Katika jimbo jengine la kusini magharibi la Sichuan, Watu wapatao 80,000 wamehamishwa, huku mvua kubwa ikisababisha Watu 300 kupoteza maisha katika Jimbo la Henan mwezi uliopita.

Leave A Reply