The House of Favourite Newspapers

Maambukizi ya wadudu kwenye mfumo wa mkojo

0

UrinaryTractInfection.jpg(Urinary Tract Infection U.T.I)

InakadiRiwa kwa asilimia 20 ya wanawake hupatwa na maambukizi katika mfumo wa mkojo, hali inayojulikana kitaalam kama Urinary Tract Infection (U.T.I) katika kipindi chote cha maisha yao hapa duniani .

Ugonjwa huu unaweza kumshambulia mgonjwa na akaona ni kitu cha kawaida na kutochukua hatua ya kwenda hospitali hadi pale  hali itakapokuwa mbaya ndipo aende kuonana na daktari.

Tabia hiyo husababishwa na wadudu wanaosababisha  U.T.I kuchelewa kuonesha dalili za ugonjwa mapema, hivyo basi, wadudu wa U.T.I huendelea kuzaliana na kuweza kuleta madhara katika mfumo wa mkojo ikiwa ni pamoja na figo.

Kuwa kuanzia mtoto anapozaliwa hadi kufikisha miaka 11 ni asilimia moja ya wavulana huwa wamepata maambukizi ya UTI na asilimia tatu kwa watoto wa kike.

Kwa wanawake huambukizwa mara 10 zaidi ya wanaume ingawaje  kwenye miaka ya zaidi ya 55 huwa maambukizi ni sawa kati ya mwanaume na mwanamke.

Pia maambukizi kwa mama wajawazito ni zaidi ya mara 10 ya wanawake ambao hawana ujauzito.

Sababu zinazochangia maambukizi ya UTI ni njia ya mkojo kuwa fupi Short Urethra kwa wanawake, hii huwa rahisi wadudu kuingia kwenye mfumo wa mkojo hasa pale mama anapokuwa na kiasi kidogo cha Hormone ya Oestrogen.

Kufanya mapenzi pia husababisha wadudu kupanda kutoka kwenye viungo vya uzazi hadi kwenye kibofu cha mkojo .

Kubana mkojo kwa muda mrefu nalo ni tatizo na inashauriwa kutofanya hivyo, ili kupunguza uwezekano wa maambukizi katika mfumo  wa mkojo.

Mpira wa kutolea mkojo

Hii husababisha wadudu kusafiri kutoka sehemu ya nje na kuingia  kwenye kibofu cha mkojo. Hali hii hutokea  kwa asilimia zaidi ya 50 kwa wagonjwa watakaokaa na mpira kwa zaidi ya siku nne.

Kwa akina mama kuacha kuona siku za hedhi Menopausal; kipindi hicho Oestrogen hupungua na kusababisha kinga ya mwili kushuka. Pia yapo magonjwa yanayopunguza kinga ya mwili kama kisukari na Ukimwi.

Njia ambazo wadudu hupitia ili kusababisha ugonjwa

Wadudu hupanda kutoka ukeni au kwenye maeneo ya haja kubwa na kuingia ndani ya viungo nya mfumo wa mkojo Ascending na kuweza kuzaliana na kusababisha ugonjwa, njia nyingine ni kupitia kwenye mfumo wa mwili wa kuchuja wadudu ili wasishambulie lympatlc.

Wadudu pia huweza kupitia kwenye damu Haematogenous na kwenda hadi kwenye figo na kwenye tumbo.

Dalili za U.T.I

Mgonjwa anaweza asiwe na dalili yoyote lakini akipima ugonjwa huu ukaonekana.

Dalili kuu ni kuhisi maumivu wakati wa kukojoa Dysuria, kusikia kukojoa mara kwa mara na mkojo kutoka kidogo kidogo, kwa mwanaume  anaweza kusikia maungo yake ya kiume yanauma wakati akiyashika pia anaweza kuona majimaji meupe kwenye tundu la mkojo, pia mwanamke anaweza kutokwa na uchafu sehemu za siri au kusikia maumivu chini ya kitovu kwenye kibofu cha mkojo.

Dalili nyingine ni homa hasa kwa watoto, joto la mwili huweza kupanda na kudhania mtoto ana malaria, dalili zingine ni kuumwa na mgongo hasa asubuhi, mwili kuchoka na kukosa hamu ya kula, pia maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Leave A Reply