The House of Favourite Newspapers

Mabondia Ndonga za Global TV Watambiana, Kupasuana Jumapili

0
Ustaadh wa kwanza kushoto, Craig Roussean na Stephen Mawenzi katika picha ya pamoja.

 

Homa ya Pambano ya ubingwa wa Global Tv, Afrika Mashariki na Kati imeendelea kupamba moto kufutia mabondia hao kutambiana wakati wakitambulishwa kwa ajili ya pambano hilo litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Dar Live  uliopo Mbagala Zakhem, Dar huku likitarajia  kurushwa mubashara  Global TV.

 

Nasibu Ramadhan na Yohana Banda wakitambiana.

 

Katika mapambano hayo Tanzania itawakalishwa na Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’, atakayezichapa dhidi ya Israel Kamwamba kutoka nchini Malawi, Nasibu Ramadhani anatarajia kuonyeshana umwamba ndani ya uringo na MMalawi, Yohana Banda huku Pialali akitarajia kupeana vitasa vya aina yake na Champion raia wa DR Congo.

 

Mratibu wa Global TV, Juma Mbizo akiwa amewanyanyua mikono mabondia Nasibu Ramadhan na Yohana Banda mbele ya waandishi wa Habari leo.

 

Mabondia hao wameonyesha kupaniana kuelekea katika ndonga hizo zitakazofanyika keshokutwa Jumapili kutokana na kila mmoja kutambia mwenza akionyesha atamchapa kwenye raundi za mwanzoni.

 

Bondia Idd Pialali (kushoto) akitambiana mpinzani wake Regin Champion kutoka DR Congo.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania, (TPBO) Yassin Abdallah ‘Ustaadh’ alisema  balozi huyo wa Malawi amekubali kuwa  mgeni rasmi katika pambano hilo ambalo litaambatana na burudani  ya muziki wa Bongo Fleva.

 

Mratibu wa Global Tv, Juma Mbizo katikati akiwatambulisha mabondia Idd Pialali na Regim Champion mbele ya waandishi wa Habari mapema leo

“Mabondia wanatarajia kupima uzito kesho Jumamosi kwa ajili ya ndonga za  kuwania ubingwa wa Global TV, lakini kikubwa kuwa Balozi wa Malawi amekubali mwaliko wa kuwa mgeni rasmi pia atakuwa akitoa sapoti kwa kijana wake, Israel Kamwamba atakayezichapa na Francis Miyeyusho.

 

Bondia Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ kuushoto akitambiana mpinzani wake Israel Kamwamba wa Malawi.

 

“Kitu kingine kikubwa ni kuwa kamati imepokea maombi ya wadau kutaka kuja ukumbini sasa tumekubali kuweka kiingilio cha sh.5000 pekee kwa sababu suala la kurusha live lipo kama lilivyo na tunategemea kuwa na wasanii wa Bongo Fleva kwa ajili ya kutoa burudani ambao ni Pam D, Wakali Dancers, Snura, Mr Dox na Dalada.”  alisema Ustaadh.

 

Katika hatua nyingine, mashabiki wataweza kulishuhudia pambano hilo mubashara kupitia simu zao za mkononi kwani litaoneshwa na Global TV pekee. Wadau na mashabiki watakaopata nafasi ya kuingia ukumbini wataingia kwa kadi maalum za mwaliko.

Bondia Regin Champion akiongea mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani

 

Ili kulishuhudia pambano hilo kwa njia ya simu tena bure, hakikisha unajiunga (SUBSCRIBE) na YouTube Channel ya Global TV Online sasa hivi ili usipitwe. Ingia YouTube, tafuta GLOBAL TV ONLINE, kisha bonyeza neno SUBSCRIBE pia bonyeza kikengele kidogo kilichopo pembeni yake ambacho kitakukumbusha kuangalia pambano hilo mara tu litakapoanza.

 

Mabondia kutoka nje wakifutilia kwa umakini

 

Kama wewe umeshajiunga, basi hakikisha pia umebonyeza kikengele ili usipitwe na kila kinachoendelea Global TV. Pia unaweza kutupata kupitia mtandao wa www.globaltvtz. com, jiunge sasa na Global TV ili uwe wa kwanza kuona ndondi za kimataifa. Kajiunge sasa kwa kuingia www.youtube.com/user/ uwazii.

 

Mkutano ukiendelea

 

 

PICHA NA RICHARD BUKOS, STORI NA IBRAHIM MUSSA | GLOBAL TV

Leave A Reply