The House of Favourite Newspapers

Mabosi Yanga Washusha Mbadala Wa Fei Toto, Fundi wa Kupiga Mashuti nje ya Boksi

0
Marouf Tshekai

TAARIFA kutoka DR Congo zinaeleza kuwa Klabu ya Yanga ipo katika mazungumzo na Klabu ya AS Vita kwa ajili ya kumsajili kiungo fundi kutoka ndani ya timu hiyo anayefahamika kwa jina la Marouf Tshekai, 26.

Kiungo huyo fundi mwenye uraia wa Togo ameshinda tuzo ya kiungo bora wa Ligi ya DR Congo kwa misimu miwili mfululizo huku akisifika kwa uwezo wake mkubwa wa kupiga mashuti nje ya boksi.

Taarifa ambazo limezipata Championi Jumatatu kutoka katika chanzo cha ndani kutoka DR Congo, zinasema kuwa Yanga ipo katika mazungumzo na viongozi wanaomsimamia mchezaji huyo ambaye inasemekana kuwa amegoma kuongeza mkataba ndani ya timu hiyo kutokana na ofa mbalimbali anazozipata kutoka klabu mbalimbali ikiwemo Yanga.

“Yanga ni kweli wamekuwa kwenye mazungumzo na viongozi wa mchezaji huyo ni kwa namna gani wanaweza kumpata katika dirisha hili dogo la usajili, Marouf ni moja kati ya wachezaji bora ndani ya ligi ya DR Congo kutokana na kushinda tuzo mbili mfululizo za kiungo bora.

Kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’.

“Viongozi wa mchezaji wanashinikiza mchezaji huyo kutokuongeza mkataba wake ndani ya AS Vita kutokana na ofa nyingi wanazopata viongozi wa mchezaji huyo wanaomsimamia ikiwemo ofa ya Yanga,” kilisema chanzo hicho.

Naye meneja wa AS Vita, Dyba Ilunga aliliambia Championi Jumatano kuwa: “Kam ni Yanga wanamhitaji mchezaji huyu wanafahamu nini cha kufanya. Yanga wanauhusiano mzuri na AS Vita na mara kadhaa wamekuwa na mawasiliano na Rais Bestine Kazadi hivyo siwezi kuzungumza chochote kwa kuwa ni jambo ambalo bado halijatokea.”

Yanga kwa sasa wanahusishwa kwa karibu na usajili wa kiungo wa kati kutokana na Feisal ambaye hucheza kwenye eneo la kiungo kuomba kuondoka ndani ya timu hiyo, ukiachana na Feisal pia Yanga wanahusishwa na kumtaka kiungo Bobosi Byrahunga.

Stori na Marco Mzumbe, Championi Jumatatu.

KAULI ya PHIRI KUHUSU MAGOLI ya MAYELE, NTIBAZONKIZA KUTUA SIMBA…

Leave A Reply