The House of Favourite Newspapers

Waziri wa Maliasili na Utalii Asisitiza Watanzania Kutembelea Vivutio vya Utalii

0
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi, Dkt Pindi Chana.

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi, Dkt Pindi Chana, ameendelea kuhamasisha wananchi kutembelea vivutio vya utalii vilivyo katika maeneo mbalimbali hapa nchini katika msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Huku yeye mwenyewe akishiriki kwa vitendo kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadani iliyoko Bagamoyo mkoani Pwani.

Akiwa katika hifadhi hiyo Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa wito kwa wananchi waendelee kulinda na kutunza vivutio vya maliasili ambavyo Tanzania imejaaliwa ili viendelee kuwa na manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Amesema Hifadhi ya Taifa ya Saadani ina vivutio vingi na vya kipekee zikiwemo fukwe za Bahari ya Hindi pia inafikika kwa urahisi kutokana na uwepo wa miundombinu rafiki kama vile reli iliyopita katika hifadhi inayowezesha watalii kufika vyema na kujionea vivutio mbalimbali.

MANDONGA ATAMBULISHA ‘PISI KALI’ YAKE BAADA YAKUSHINDA ARUSHA..

Leave A Reply