The House of Favourite Newspapers

Madenti Wapatwa na Gonjwa la Ajabu

0

Stori: Francis Godwin, Kilolo

WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Mhanga Kata ya Kimara Wilaya ya Kilolo wamekumbwa na ugonjwa wa kuanguka hovyo kwa zaidi ya miezi sita sasa chanzo kikitajwa kuwa ni vijiti vya ajabu vilivyokutwa mfukoni mwa mwanafunzi mmoja msichana anayesoma darasa la saba.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Zamoyoni Mvella akitoa taarifa ya kuanguka kwa wanafunzi hao mbele ya Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto hivi karibuni, alisema tatizo hilo la wanafunzi kuanguka limekuwa likijitokeza kila siku kwa zaidi ya miezi 6 sasa mfululizo na kuwa idadi ya siku moja kwa wanafunzi kuanguka ni kati ya 8 hadi wanafunzi 16.

Alisema kuwa tatizo hilo lilianza kwa mwanafunzi mmoja wa darasa la saba aliyemaliza mwaka jana ila kwa sasa limeendelea kwa kasi kutoka mtoto mmoja hadi kufikia watoto zaidi ya 15 kwa siku.
Mkuu huyo alisema kuwa wanafunzi wanaoongoza kuanguka zaidi ni wasichana huku wavulana ni mtoto mmoja pekee na kuwa jitihada za uongozi wa shule hiyo ambazo zimefanyika ni pamoja na kutoa taarifa kwa viongozi wa elimu ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na kuwaita wazazi wote wa wanafunzi ili kuona namna ya kulikabili.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Emelius Kihongosi alikiri kutokea kwa tatizo hilo na kusema wanafunzi hao wanasumbuliwa na mapepo.

Leave A Reply