The House of Favourite Newspapers

MADRID: TUPENI POGBA TUWAPE BALE

 

Paul Pogba.

REAL Madrid imeamua kuchukua maamuzi ya kumuingiza sokoni winga wake, Gareth Bale mwishoni mwa msimu huu na atakuwa anapatikana kwa pauni milioni 113.

Hatua hiyo imekuja baada ya kudumu kwa misimu sita na kutwaa mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini bado Bale ameonekana kutokuwa kipenzi cha mashabiki wa Madrid.

 

Kumekuwa na taarifa kuwa anatarajiwa kurejea England kucheza katika Premier League na klabu inayotajwa ni Manchester United ambapo Madrid ipo tayari kumtoa kwa kubadilishana na Paul Pogba.

 

Imeelezwa kuwa Real Madrid ipo tayari kumtoa Bale kwa kiwango hicho cha fedha lakini pia anaweza kutumika katika mpango wa kubadiliashana na Pogba ambaye ameonyesha wazi anataka kwenda Madrid.

 

Imeshajulikana wazi kuwa licha ya kuwa bado ana mkataba wa muda mrefu, lakini Bale hayumo katika mipango ya muda mrefu ya kocha wa sasa wa Madrid, Zinedine Zidane.

Hivyo, ikiwa presha itakuwa kubwa, United wanaweza kukubali kumsajili Bale kisha kumruhusu Pogba aondoke kwa kuwa tayari kuna taarifa hana uhusiano mzuri na kocha wake wa sasa kutokana na nia yake ya kuonyesha anataka kuondoka.

 

Bale ameichezea Madrid mechi 227 na kufunga mabao 102 tangu alipojiunga na timu hiyo kwa pauni milioni 85.3, Septemba 2013 akitokea Tottenham.

Comments are closed.