The House of Favourite Newspapers

Mafao ya Wastaafu Yalivuruga Bunge – Video

0

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Novemba 3, 2021 limechachamaa huku likiitaka Wizara ya Utumishi kuhakikisha wanawalipa mafao yao kwa wakati wastaafu wastaafu wanaomaliza muda wao wa kulitumikia Taifa.

 

“Hili suala la wastaafu ni kero kubwa, wastaafu wanaolia na wanaokwenda kwenye maofisi miezi sita, hadi miaka mitano ni wengi, serikali itafute mfumo thabiti wapate fedha zao, watu wanakufa wanadai hela zao, kwanini mtu ametumikia nchi afe anadai hela?”- Mwita Getere.

 

“Wakati mwingine ucheleweshaji wa mafao ya wastaafu yanatokana na malimbikizo ya michango inayotakiwa kupelekwa na waajiri, tumekuja na suluhu ya kutengeneza mfumo wa kutambua lini wanastaafu na haki zao zikoje,”- Waziri Jenista Mhagama.

 

“Kwenye Bunge la bajeti, Waziri aliji-commit kwamba atafanya ziara kwenye vyombo vyote vya habari kuhakikisha waajiri wanapeleka michango ili waandishi wa habari na watu wengine binafsi walipwe kwa wakati, ni lini sasa ataanza hiyo ziara?,”- Esther Bulaya.

.

“Mtu anayestaafu leo na miaka 60 maana yake amezaliwa mwaka 61 na kama alianza kazi na miaka 20 maana yake miaka ya 70 ndiyo alianza kazi, anapostaafu tu anaanza kufuatilia mafao anaambiwa kalete barua yako ya ajira na ya uthibitisho wa kazi ya mwaka 72” – Spika Ndugai.

 

“Kwahiyo yako maeneo ya kuangalia visiwepo visababu, watu wengi wanakosa haki zao sababu hiyo kwamba aliajiriwa Muleba anamaliza kazi yake Tandahimba anaanza kuambiwa kalete ile karatasi yako ya Muleba uliyoanza kuajiriwa,”- Spika Ndugai.

 

Leave A Reply